Saturday, February 9, 2008

UHUSIANO KATI YA WAZAZI NA WATOTO

Familia nyingi hapa Tanzania zimekuwa hazielewi au zimekuwa zikiwaweka mbali watoto wao katika masuala mbalimbali ya kifamilia, baba anakuwa mkali hataki kuwa wazi kwa sababu anahofia atamharibu mtoto wake. Hivyo watoto wanapokuwa wakubwa wanakuwa waoga kuwaeleza wazazi wao hisia zao au jinsi gani ya kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayowakumba.

Matokeo yake itapeleke mtoto anakua katika hali ya kutojiamini, kwa maana anahisi hakuna anayemwamini, hakuna anayemuelewa na hakuna atakayeweza kumsikiliza. Anafanya mambo kwa siri na anatumbukia katika mitego mbalimbali ambayo haaweza kujinasua.

Tukirudi kwa wazazi, wanadhani kwa kuwalea watoto wao hivyo wanafikiri wanawapenda na wanawalea katika maadili mema ya heshima au kuwaheshu wakubwa au kutozungumza masuala fulani fulani kwa wakubwa hasa wana vunja ungo au kubalehe, wanapoingia katika mahusiano wanaposhindwa katika mitihani, Nadhani wazazi ni muda wa kufikiria na kujaribu kuwa marafiki na watoto hii itawasaidia kujiamini na kuwa huru kujisimamia katik amaamuzi yao binafsi.

Kwa sababu mtoto atajua dhahiri kwamba ninaye rafiki ambaye pia ni mzazi wangu hivyo nitamueleza jinsi ninavyojisikia. Lakini kwa kuwatenga watoto kunaleta uadui na kujifunza au kurithi tabia mbaya atakapokuwa mbali na nyumbani.

Karibuni

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home